Mbona Common Voice?
Teknolojia inayotambua sauti inazidi kuenea - kuanzia wasaidizi wa simu janja hadi vifaa vya huduma za afya vinavyovaliwa hadi programu ya kujifunza lugha. Pia inawaacha watu wengi nyuma. Visaidizi vya sauti kwa sasa vina chini ya 1% ya lugha za ulimwengu! Katika jamii zingine, hata kama lugha yao inatumika, huenda isieleweke kwani data ya mafunzo ya AI mara kwa mara haiwakilishi jamii zenye jinsia mbalimbali, Watu wasio Wazungu na walio na lafudhi zilizotengwa au zisizo za asili.
Tuko hapa ili kubadilisha jambo hilo! Kwa kuhakikisha kuwa ni rahisi kwa watu kama wewe kushiriki sauti yako.
Je, Common Voice hufanya kazi vipi?
- Hatua ya 1. Mtu anaomba lugha iongezwe.
- Hatua ya 2. Maandishi ya tovuti inatafsiriwa katika lugha hiyo na watu wanaojitolea.
- Hatua ya 3. Sentensi inakusanywa ili watu wasome kwa sauti.
- Hatua ya 4. Tunazindua jukwaa la Common Voice katika lugha hii.
- Hatua ya 5. Watu wanakuja na kuchangia sauti zao.
- Hatua ya 6. Watu wengine wanathibitisha makala hayo ya sauti.
- Hatua ya 7. Tunatoa seti hiyo ya takwimu kila baada ya miezi 3.
- Hatua ya 8. Mafuatano yanaendelea! Sentensi nyingi zaidi, makala mengi zaidi, uthibitisho mwingi zaidi! Daima tunahitaji msaada wako!
Kwa hivyo ninajihusishaje?
Asante kwa kuuliza! Angalia kwenye tovuti ili uone ikiwa lugha yako inahitaji makala mengi zaidi, uthibitisho mwingi zaidi, au sentensi nyingi zaidi.
Kama huna uhakika - usisite kuchangia baadhi ya makala! Inachukua dakika chache tu kuhakikiaha kuwa AI inamfaa kila mtu.
Ikiwa unataka kujihusisha zaidi, kwa nini usiwe mhamasishaji wa jamii - kuacha kuwa mwalimu wa masuala ya ujumuishaji wa AI mtandaoni na kuendesha shughuli za matukio ya jamii yako - kuna njia nyingi za kusaidia! Wasiliana nasi tu na tutawasiliana na watu sahihi wa kukusaidia.
Ni nini kinachofuata katika jukwaa la Common Voice!
Katika upande wa uzoefu wa wachangiaji, kwa sasa tunajitahidi ili kuhakikisha kuwa watu walio katika mazingira yenye kipimo data cha chini wanaweza kutumia jukwaa kwa urahisi na kulifanya liwe rahisi kwa watu wapya kushiriki haraka. Katika usanifu wa programu na miundombinu, tunafanya jukwaa liwe bainifu zaidi na kipimo data kuwa linaloweza kugawanywa kwa watumiaji wa data.
Mwaka ujao, tutakuwa tukifanya mabadiliko makubwa ya jukwaa - ikiwa ni pamoja na kuongeza mazungumzo ya hiari. Ikiwa wewe ni mhandisi au mwanasayansi wa data ambaye anataka kusaidia - wasiliana nasi!