Common Voice

Common Voice ndio seti ya takwimu iliyo na lugha nyingi tofauti zaidi duniani. Takwimu nyingi za sauti zinamilikiwa na makampuni yanayozuia uvumbuzi. Hayawakilishi vizuri takriban lugha zote ulimwenguni, watu wasio wazungu, walemavu, wanawake na jumuiya ya LGBTQIA+. Tunataka kubadilisha hilo kwa kuhamasisha watu kila mahali kushiriki sauti zao.

Kazi ya programu

Je, washirika wa Mozilla wa Common Voice ni akina nani?

Washirika wa Mozilla ni wanaharakati, watafiti wanaotumia taarifa za umma, wahandisi, na wataalamu wa sera za teknolojia wanaofanya kazi kwenye mstari wa mbele wa harakati hiyo. Washirika hubuni mawazo mapya juu ya jinsi ya kukabiliana na vitisho vinavyojitokeza na changamoto zinazokabili mtandao wenye maadili mema. Washirika wanne kutoka Rwanda, Kenya na Tanzania wamechaguliwa kama viongozi katika nafasi ya teknolojia ya sauti huria zilizo katika jamii zetu lengwa. Washirika hawa wamekuza jukwaa, wameunganisha mradi huo na wadau mbalimbali na wamehamasisha thamani ya kuwekezaji zaidi katika Lugha za Kiafrika.

Kutana na washirika wa Kiswahili wa 2021/2022

Britone Mwasaru

Britone Mwasaru atatumia teknolojia ya sauti kwa kuzingatia lugha ya Kiswahili ili kushughulikia watu ambao lugha yao ya kwanza au inayopendelewa ni Kiswahili waliotengwa. Kabla ya kujiunga na Mozilla, Britone alikuwa Mkurugenzi wa Teknolojia katika Swahilipot Hub ambapo aliongoza matumizi na kupitishwa kwa teknolojia katika jamii ya teknolojia na sanaa jijini Mombasa na eneo la Pwani mwa Kenya.

Kathleen Siminyu

Kathleen Siminyu ni Mtafiti wa AI ambaye ameangazia Uchakataji wa Lugha Asilia wa Lugha za Kiafrika. Atajiunga na shirika la Mozilla Foundation kama Mshirika wa Kujifunza kwa Mashine ili asaidie kutengeneza seti ya takwimu ya Common Voice ya Kiswahili na aunde mifano ya kunukuu usemi ili itumiwe katika nyanja za kilimo na usimamizi wa fedha. Katika utafiti wake wa NLP, Kathleen amewahi kufanya kazi ya kunukuu usemi kwa lugha za Kiluhya na kuchangia katika tafsiri ya mashine ya lugha za Kenya kama sehemu ya Masakhane. Kabla ya kujiunga na Mozilla, Kathleen alikuwa Mratibu wa Kanda wa AI4D Afrika, ambapo alifanya kazi na jumuiya za ML na AI barani Afrika akiendesha shughuli za mipango mbalimbali.

Rebecca

Rebecca atakuwa akifanya kazi ya kuanzisha na kusaidia jamii mbalimbali za lugha ya Kiswahili na teknolojia kwa kuzingatia jinsia, umri, asili, lafudhi na lugha za kienyeji ili kujenga seti ya takwimu ya sauti huria katika Kiswahili. Atahakikisha kuwa seti ya takwimu inawakilisha vizuri watu wanaozungumza Kiswahili akiwa na lengo la kuhamasisha utumiaji na utekelezaji wa teknolojia ya sauti. Kabla ya kujiunga na Mozilla, Rebecca amekuwa mshirika wa Internet Society, mshirika wa Afrisig, mshirika wa Google Policy, mtafiti wa national geographic na afisa wa mpango wa haki za kidijitali katika Mpango wa Paradigm.

Soma zaidi kuhusu Ushirikiano wa Mozilla hapa.

Mifano ya Tuzo za Mozilla Common Voice za Kiswahili

Common Voice imetunuku miradi minane kila mmoja dola 50,000 za Marekani, kwa kutumia lugha ya Kiswahili na teknolojia ya sauti ili kuongeza fursa za kiuchumi kwa makundi yaliyotengwa nchini Kenya, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumza Kiswahili.

Ruzuku hizi zinatolewa na shirika la Gates Foundation likishirikiana na Ofisi ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo (FCDO) na GIZ, kama mwitikio wa mbinu unaozingatia jinsia na jamii katika maendeleo ya teknolojia.

Soma tangazo la ruzuku hapa

Kutana na wapokeaji wa tuzo:

ChamaChat
ChamaChat na Ujuzi Craft LTD | Kenya

Mfumo wa usimamizi wa Chama wenye chatboti au programu inayoiga mazungumzo na inayoshirikisha mazungumzo baina ya wanachama na kutoa majibu ya sauti kwa Kiswahili kupitia Ujumbe mfupi (SMS)na Whatsapp. Inaunganishwa na kiolesura cha programu-tumizi ya Malipo ya kikundi, yaani API ya M-Pesa. Wanachama wanaweza kushirikiana na chatboti ya msimamizi wa Chama kwenye utendaji kazi mbalimbali, ikijumuisha kuangalia salio, maombi ya mkopo na kupokea taarifa za akaunti.

Kiazi Bora
Kiazi Bora ya Sustain Earth's Environment Africa | Tanzania

Kiazi Bora, hutumia programu ya sauti inayowafahamisha wanawake wanaoishi katika mazingira magumu na wanaoishi katika maeneo ya vijijini na jamii zilizotengwa za Tanzania kuhusu thamani za lishe ya Viazi vitamu vyenye rangi ya chungwa/njano (OFSP), ujuzi wa kilimo ili kupata mazao bora, na upatikanaji wa soko wa kina wa bidhaa za chakula ghafi au zilizosindikwa za OFSP, kupitia programu ya seti ya data ya sauti.

Jifunze zaidi kuhusu Kiazi Bora.

Wezesha na Kabambe
Wezesha na Kabambe ya Chuo cha Westminster, U.K| Chuo cha Moi, Kenya| Chuo cha Kiufundi cha Kenya | Chuo cha Western Michigan, USA.

Ni boti ya sauti ya Kiswahili ya simu ya mkononi ambayo haitegemei muunganisho wa intaneti. Imeandaliwa kwa ushirikiano na wakulima wadogo wanawake wa vijijini nchini Kenya kama chanzo mbadala cha taarifa za kilimo. Kwa kutumia seti za data za Mozilla katika Kiswahili, boti hii ya mazungumzo ya simu ya mkononi inaweza kutumika kwenye simu za kawaida (kabambe) na simu janja na wakulima wadogo vijijini. Boti hii shirikishi ya Kiswahili inaendeshwa na hifadhidata ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutoka kwa wakulima wadogo wadogo wanawake, kikundi kilichotengwa kidijitali. Imechochewa na ujuzi uliopo, kukubalika kwa teknolojia za simu katika maeneo ya mashambani nchini Kenya.

Jifunze zaidi kuhusu Wezesha na Kabambe.

LivHealth Kiswahili Corpus
LivHealth Kiswahili Corpus ya Badili Innovations | Kenya

LivHealth Kiswahili Corpus inalenga kuwezesha jamii kutambua kwa usahihi magonjwa ya mifugo na kupata afua kwa wakati kutoka kwa watendaji waliohitimu. Kwa kutumia Uchakataji wa Lugha Asilia (NLP), Kujifunza kwa Mashine (ML), na Akili Bandia (AI), mradi utajenga miundo ya Kiswahili ya maandishi-hadi-sauti kwa ajili ya kusambaza taarifa za magonjwa kwa jamii zilizotengwa. Wakifanya kazi kwa karibu na washirika wao, Kituo cha One Health Center in Africa(OHRECA) chenye makao yake ILRI, wataimarisha utendaji wa mfumo wa LivHealth ili kuwezesha jamii za wenyeji kupata taarifa hitajika za magonjwa kwa urahisi na kwa Kiswahili.

Imarika
Imarika ya Chuo cha Strathmore | Kenya

Imarika ni boti ya mazungumzo inayotoa huduma za ushauri wa hali ya hewa kidijitali katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili ambayo itasaidia wakulima wadogo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mradi huu unalenga kukabiliana na hatari ya wakulima kukabiliwa na hali ya hewa isiyotabirika kutokana na kukosekana kwa utabiri wa hali ya hewa unaoweza kufikiwa, wa kutegemewa na wa eneo. Upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa ni tofauti sana katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa kawaida ni utabiri wa hali ya chini ya usahihi wa kitaifa au wa kikanda unaotangazwa kwenye redio na/au TV. Mradi hasa unatarajia kuwahudumia wakulima wadogo ambao mara nyingi wana ufikiaji mdogo wa huduma za ushauri wa hali ya hewa zilizowekwa ndani kutokana na vizuizi kama vile kupenya polepole kwa teknolojia au kutojua kusoma na kuandika kwa dijiti.

Jifunze zaidi kuhusu Imarika.

Paza Sauti
Paza Sauti ya Tech Innovators Network Ltd | Kenya

Mradi huu unatengeneza boti ya mazungumzo na huduma ya mwingiliano ya mwitikio wa sauti ambayo itatoa huduma zinazowezeshwa kwa sauti katika kikoa cha usajili wa biashara na kuongeza ufahamu kuhusu matumizi ya dhamana (usalama) kuwezesha kupata mkopo nchini Kenya. Lengo kuu ni kuongeza ujuzi wa kifedha kuhusu mali zinazohamishika kama dhamana, hasa kwa wanawake katika biashara, na hasa kilimo, kwa madhumuni ya kupata mikopo. Ingawa kumekuwa na ongezeko la urahisi wa kupata mikopo, wananchi wengi bado hawajui uwezo wao wa kupata mikopo zaidi kutokana na kutumia mali zinazohamishika kama dhamana. Mradi huu utakuwa mwendelezo wa ushirikiano unaoendelea tayari na Business Registration Service - BRS (Shirika la serikali) nchini Kenya katika kikoa cha ujumuishaji wa kifedha, ambacho huhudumia umma wa Kenya.

Jukwaa la Utambuzi wa Maandishi ya Kiswahili na Sauti (KTVRP)
Kiswahili Text and Voice Recognition Platform (KTVRP) kwa Ushauri wa Kilimo na Huduma za Kifedha kwa Wakulima Wadogo ya Duniacom Group, LLC| Tanzania / Marekani

Wengi wa wakulima wadogo nchini Tanzania wana uwezo wa kuwasiliana kupitia lugha ya Kiswahili na lahaja zake pekee. Jukwaa la maandishi na sauti linalopatikana katika lugha ya watu wasiohudumiwa (yaani, Kiswahili) litakuwa ufunguo wa ufikiaji mpana, kupitishwa na matumizi ya ushauri wa kidijitali ya kilimo na huduma za kifedha nchini Tanzania. Lengo ni kuandaa jukwaa la utambuzi wa maandishi na sauti ambalo litawapa wakulima wadogo katika mnyororo wa Thamani wa Mahindi Tanzania na huduma za kidijitali za kifedha na zisizo za kifedha za kiotomatiki kwa kuzingatia eneo, maeneo ya ikolojia ya kilimo na mzunguko wa mazao. Kulingana na data iliyogawanywa kwa jinsia kutoka kwa awamu ya majaribio, inategemewa kuwa wengi wa washiriki watakuwa wanawake.

Jifunze zaidi kuhusu KTVRP.

Haki des femmes
Haki des femmes ya Core23Lab | Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

Haki des femmes itatumia teknolojia ya sauti kutoa ufikiaji wa taarifa za kisheria na usaidizi kwa wanawake katika majimbo ya Katanga na Lualaba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuhakikisha wana haki ya kupata, kutumia, kurithi, kudhibiti na kumiliki ardhi. Wanawake wengi nchini DRC mara nyingi hupoteza uwezo wao wa kumiliki ardhi baada ya kufiwa na wapendwa wao au waume zao kutokana na kukosa ufahamu wa haki za ardhi. Suluhu hili itasaidia wanawake kupata taarifa na usaidizi wa kisheria katika kupata haki zao za ardhi kwa lugha ya Kiswahili.

Jifunze zaidi kuhusu Haki des femmes.