Jamii, uhamasishaji na utawala
Jamii ni moyo wa Common Voice- harakati yetu inaendeshwa na watu nusu milioni duniani kote.
Je, tunamaanisha nini tunaposema Jamii?
Swali nzuri. Jamii ni mfumo wa kushangaza wa wasanii, wahandisi, wanaharakati, wanasayansi wa data, waandaaji na watafiti ambao huchangia wakati wao kutekeleza shughuli za Common Voice. Baadhi ya jamii zetu zimeunganishwa sana - zinatumia muda pamoja, mtandaoni na ana kwa ana - jamii zingine zinapendelea kuangalia kwa karibu na kuchangia mara kwa mara bila kuzungumza sana. Tunakaribisha kila mtu!
Je, jamii hufanya nini?
Kila mwanajamii ni tofauti - wengine huchangia msimbo wa kufanya jukwaa kuwa bora, wengine hujenga mambo kwa seti ya takwimu na wengine hujenga ushirikiano wa sentensi za maandishi ya watu wote. Watu ambao wamekuwa katika jamii kwa muda mrefu wanaweza kusaidia katika kujumuisha lugha mpya kwa kujibu maswali katika vikao vyetu, au kuzungumza katika matukio ili kueneza neno! Tunahitaji kujitahidi sana ili tufikie lengo letu la kuwa na teknolojia salama, inayojumuisha lugha ya kila mtu. Ikiwa una ujuzi au wazo na huna uhakika jinsi ya kulitumia - wasiliana tu na timu yetu ya jamii!
Soma zaidi
Blogu juu ya kazi ya uhamasishaji na Washirika wa Kiswahili
Jihusishe!
Hotuba | GitHub | Matrix | Barua pepe | Kijitabu cha Jamii