Kwa nini tunatoa ruzuku
Intaneti ina uwezo wa kuinua jamii — inaweza kukuza demokrasia, masoko huria, na uhuru wa kujieleza. Lakini pia inaweza kukuza ubaguzi, ufuatiliaji wa watu wengi, na habari potofu.
Kuliko wakati mwingine wowote, tunahitaji harakati za kuhakikisha kuwa mtandao unaendelea kutumiwa kwa kusudi zuri. Ushirika na Tuzo za Mozilla zinachochea harakati hii kwa kuunga mkono vitendo vya kibinafsi na vya pamoja vinavyoendeleza mtandao unaozingatia binadamu zaidi. Tunatoa fedha, ushauri, na kusaidia wavumbuzi wa kila aina — kuanzia wataalamu wa teknolojia na wanasayansi hadi wanaharakati na wasanii. Kwa upande wao, watu hawa wanajaribu mitaala ya sayansi ya kompyuta yenye maadili katika vyuo vikuu vinavyoongoza. Wanafuatilia kuenea kwa taarifa potofu mtandaoni na kuwasilisha matokeo yao kwa watunga sera wakuu wa Marekani. Wanaunganisha watu wasio na mtandao wa intaneti vijijini Tanzania kwa kutumia teknolojia ya white-space ya televisheni. Na mengi zaidi.
Washirika wa Mozilla huleta mabadiliko
Kile tunachofadhili
Mozilla hupata, husaidia, na huunganisha washirika wa harakati kujenga AI huria, jumuishi na ya kuaminika zaidi. Kupitia ushirika na tuzo, tunaunga mkono watu na mawazo ya ujasiri yanayoweza kuunda mtandao unaozingatia binadamu zaidi.
Viongozi hawa huunda teknolojia mpya, kuendeleza vifaa vya zana na mitaala, hufanya kampeni, ufumbuzi wa mfano, na kushawishi sera duniani kote kwa:

Fikiria upya kanuni, sera, miundombinu na teknolojia mpya zinazolinda na kuwawezesha watu binafsi na jamii mtandaoni.

Tengeneza upya makundi mengi— na tofauti zaidi — katika maendeleo, usambazaji, na usimamizi wa teknolojia zinazounda mtandao.

Panga upya nguvu mtandaoni, na uwarejeshe watu binafsi na jamii nguvu hiyo.

Apply to the Mozilla Technology Fund before 5 October!
Jinsi tunavyofadhili
Mozilla inashirikiana na washirika na wasidizi ili kuchochea harakati za watumiaji wa intaneti, wasomi, wasanii, wataalamu wa teknolojia, viongozi wa mawazo, na wanaharakati wanaopigania intaneti yenye maadili mema. Ufadhili hutolewa kupitia ushirika na tuzo ili kusaidia hatua za mtu binafsi na za pamoja ili kusaidia kukuza jamii inayohusiana, kuimarisha teknolojia na mifano ibuka, na kujenga miundombinu ya muda mrefu inayohitajika kwa ajili ya mtandao huria, salama, na jumuishi zaidi.
Tuliowafadhili
Washirika wa Mozilla na Wapokeaji tuzo wanawakilisha nyanja na mazingira mbalimbali: Wao ni watunga sera nchini Kenya, waandishi wa habari nchini Brazil, wahandisi nchini Ujerumani, wanaharakati wa faragha nchini Marekani, na wanasayansi wa data nchini Uholanzi. Tunatafuta washirika na wapokeaji tuzo wanaozingatia sana dhamira yao, mabingwa katika biashara zao, na walio na mawazo mapya ya ujasiri yanayoweza kuchochea mabadiliko ya kudumu.
Anouk Ruhaak | Mshirika wa Mozilla
Anouk hujenga mifano mpya ya usimamizi wa data kwa ajili ya umma. Kama muasisi wa mipango na mtetezi wa amana za data, anakuza mifano ya usimamizi inayolinda faragha na kulinda jamii kutokana na mambo mabaya ya kushiriki data.
Survival of the Best Fit | Tuzo Iliyopita
Ilijengwa na Gabor Csapo, Jihyun Kim, Miha Klasinc, na Alia ElKattan, Survival of the Best Fit ni mchezo wa kielimu unaohusu upendeleo wa kuajiri katika AI. Inalenga kuelezea jinsi kutumia AI vibaya kunaweza kufanya mashine irithi upendeleo wa kibinadamu na kuzidisha kutokuwepo kwa usawa.
Kazi ambazo tumefadhili
Changamoto zinazokabili mtandao ni tata, na tunajua kuwa kuna suluhisho chache zinazoweza kutatua changamoto zote. Mozilla imejitolea kusaidia wavumbuzi mbalimbali duniani kote kufikiria ufumbuzi utakaosadia vyema jamii zao.
Mozilla has distributed $22 million in award funds since 2015 and supported more than 200 fellows. This funding has supported organizations and individuals in 46 countries across six continents.


Ushirika
Ushirika wa Mozilla hutoa rasilimali, jamii, na huisaidia viongozi wa maadili mema ya mtandao kujenga ulimwengu kidijitali unaozingatia binadamu zaidi.

Tuzo
Tuzo za Mozilla hutoa fedha, msaada kwa marika, na ushauri kwa miradi inayoshughulikia changamoto kubwa zaidi zinazokabili mtandao na watumiaji wake.

Nafasi ya Majiribio ya Data
Nafasi ya majaribio ya kuchochea mbinu mpya ya kushughulikia changamoto za usimamizi wa data.

Mradi wa Ukaguzi Huria (OAT)
Mradi mpya ulilenga hasa matokeo ya ukaguzi na zana, mbinu na rasilimali zinazohitajika kusaidia watu wanaohusika katika aina hii ya kazi.

Kuwa Mshirika
Washirika wetu wa ufadhili wanatusaidia kukuza mpango wetu wa ushirika na tuzo, kufikia sehemu mpya za dunia na kuchunguza makutano mapya ya mashirika ya kiraia na mtandao.