Jumuiya na Asasi za Kiraia
Jamii ndio moyo wa mradi wa Common Voice - wanatoka ulimwenguni kote, na ni wanaharakati wa lugha na watafiti na wasanii na wanasayansi wa data. Unaweza kujifunza zaidi kuhusu jinsi ya kushiriki katika ukurasa wetu unaoelezea Kutuhusu na katika kijitabu chetu cha Jamii. Ikiwa unataka ushirikiano wa ndani na shirika, wasiliana.
Mashirika
Tunashirikiana na mashirika, asasi za kiraia na washirika wa jamii kukuza maadili mema ya mtandao wa intaneti, huku tukilenga hasa Afrika Mashariki. Jifunze zaidi kuhusu kazi yetu ya programu.
Serikali
Tunafurahia kujihusisha kwa sekta ya umma katika teknolojia, uvumbuzi na haki za lugha. Ikiwa unapanga kufanya mradi au kampeni kubwa, tafadhali wasiliana nasi.
Vyuo vikuu, Wasomi na Watafiti
Uvumbuzi huria ni msingi wa kile tunachofanya. Kwa ushirikiano katika utafiti, ukusanyaji wa data au mahojiano, wasiliana nasi.
Biashara ndogo ndogo, ikiwemo teknolojia na biashara zinazoanza za AI
Daima tunatazamia kusikia kutoka kwa watumiaji wa data kuhusu mahitaji na taratibu zao - kuanzia kushirikiana katika jukwaa la kukusanya data hadi kutoa maarifa kuhusu maadili mema ya data, tunataka kusikia kutoka kwako.
Makampuni makubwa na makampuni ya jukwaa
Ikiwa unataka kuzungumza zaidi kuhusu seti ya takwimu, unataka kuwekeza pamoja katika upanzuzi wa jukwaa uliopangwa au unatafuta fursa za kushirikiana, tutumie ujumbe.