Common Voice

Sauti ya Jamii ndio seti ya takwimu iliyo na lugha nyingi tofauti zaidi duniani. Takwimu nyingi za sauti zinamilikiwa na makampuni yanayozuia uvumbuzi. Hayawakilishi vizuri takriban lugha zote ulimwenguni, watu wasio wazungu, walemavu, wanawake na jumuiya ya LGBTQIA+. Tunataka kubadilisha hilo kwa kuhamasisha watu kila mahali kushiriki sauti zao.