Mradi wa Mozilla wa Common Voice pamoja na Hekaya Arts utawatuza waandishi watatu bora wa fasihi za Kiswahili. Washindi hao watatu watatuzwa dola za Marekani 400, 250 na 100 mtawalia.

Shindano hili la uandishi ni mojawapo ya sehemu ya mradi wa Mozilla wa Common Voice unaolenga kueneza na kukuza data huria ya Kiswahili ili kuwezesha utumizi na ujumuishaji wa lugha za Kiafrika katika ujenzi wa technologia.

Hekaya Arts Initiative ni shirika la fasihi na utamaduni, ambalo linaleta mazungumzo kuhusu matumizi na maendeleo ya lugha ya Kiswahili kupitia sherehe za sanaa na fasihi.

Mashindano haya yananuia kuvutia waandishi mbali mbali kutoka maeneo mengine ambako Kiswahili kinazungumzwa, kando na Afrika Mashariki ambako Kiswahili kinazungumzwa sana. Tarehe ya mwisho ya kutoa nakala za uandishi ni Aprili 30, 2022, na washindi watatangazwa Mei 13, 2022.

Waandishi wanashauriwa kuchunguza muundo wa maandishi ya ubunifu unaoongozwa na masuala ya utamaduni na haki ya kijamii katika makundi yafuatayo:

 • Muziki/nyimbo, densi na vyombo vya kitamaduni.
 • Lugha
 • Tamaduni na Urithi.
 • Vyombo vya kitamaduni
 • Urembo na mapambo
 • Ujenzi wa nyumba / Usanifu majengo
 • Afya ya kiasili / mazoezi ya kiasili ya afya
 • Fasihi na isimu
 • Utamaduni/mbinu za kutafuta riziki za kitamaduni, k.m ufinyanzi
 • Masuala ya kijamii kama vile haki ya ardhi, makaburi ya umati, Ukristo na athari zake kwenye mazoezi ya kitamaduni
 • Watu mashuhuri/Mashujaa wa kihistoria
 • Historia na akiolojia.

Maelekezo kuhusu uwasilishaji:

 • Kazi zitakazowasilishwa zitakuwa kwenye tovuti ya umma. Zitakuwa chini ya leseni ya tovuti (CC-0) za umma.
 • Wawasilishaji lazima watie saini Makubaliano ya Uwasilishaji hapa.
 • Maelezo kuhusu nakala za uandishi:
  • Usitumie tarakimu k.m 2021, badala yake tumia maneno,
  • Usitumie maneno ya kufupishwa, k.m “USA” au “ICE” kwa kuwa huenda yakasomwa tofauti na yanavyotamkwa.
  • Nakala isitumie maneno ya kuvunja heshima.
  • Nakala isiwe yenye kuchochea aina yoyote ya unyanyasaji wa kijinsia dhuluma, au vita
  • Nakala hizi hazipaswi kuchochea au kutukuza unyanyasaji wa kijinsia au ubaguzi
  • Nakala inapaswa kuheshimu utofauti wa jinsia, yaani matumizi ya viwakilishi sahihi
  • Maneno kwenye nakala yasiwe ya kueneza vitisho na vita
  • Nakala iwasilishwe kidigitali wala sio kwa kuandikwa kwa mkono.
  • Kazi iwe yako mwenyewe, isiwe ya kuigwa.

Wasilisha kazi yako kabla ya tarehe 30 Aprili, 2022 kwa anwani ya barua pepe ifuatayo [email protected]. Kwa maelezo zaidi tembelea: Hekaya Arts Initiative


Maudhui yanayohusiana