Common Voice inatoa matangazo kuhusa dola 400,000 za Marekani za Tuzo kwa ajili ya Teknolojia ya Sauti ya Kiswahili
Mozilla Common Voice inatangaza dola 400,000 za Marekani katika misaada kwa teknolojia za sauti ambazo zinatumia data yetu ya Kiswahili ya chanzo wazi. Tuzo za hadi dola 50,000 za Marekani kila moja zitatolewa kwa miradi itakayoshinda nchini Kenya, Tanzania na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Hasa, Common Voice inatafuta miradi ambayo inazingatia kilimo na fedha, na ambayo inasaidia kuinua makundi ambayo hayana maarifa na yametengwa kidigitali. Mpango huo utasaidia watu na miradi kote Afrika Mashariki ambayo hutumia teknolojia ya sauti kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.