Tuzo za Kiswahili za Common Voice

Tuzo za Kiswahili za Common Voice

Tuzo za Kiswahili za Common Voice


Mozilla inafadhili watu na miradi kote Afrika Mashariki ambao hutumia data ya sauti huria ya Common Voice ili kufungua fursa za kijamii na kiuchumi.

Picha ya kielelezo ya jumuiya

Teknolojia ya sauti inazidi kuwa lango la intaneti - lakini teknolojia hii haitumikii kila mtu kwa usawa. Hakika, Alexa ya Amazon, Siri ya Apple, na Google Home hazihimili hata lugha moja ya asili ya Kiafrika. Hii ina maana kwamba mamilioni ya watu wanaozungumza Kiswahili na lugha nyingine za Kiafrika hawawezi kutumia teknolojia ya sauti kufanya jambo rahisi kama kuangalia hali ya hewa - au jambo muhimu kama kuangalia masasisho ya COVID.

Common Voice ya Mozilla ni mpango wa chanzo huria ili kushughulikia tofauti hii, kwa kuunda seti za data za sauti za chanzo huria katika lugha ambazo hazihudumiwi vya kutosha. Kazi nyingi za Common Voice hulenga katika kujenga seti ya data ya Kiswahili - na tuzo hizi za Kiswahili za Common Voice ni sehemu ya kazi hiyo.

Mozilla imekabidhi miradi minane dola $50,000 za Marekani kila mmoja, kwa kutumia lugha ya Kiswahili na teknolojia ya sauti kuongeza fursa za kijamii na kiuchumi kwa makundi yaliyotengwa nchini Kenya, Tanzania, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo inayozungumza Kiswahili. Tuzo hizi, zenye jumla ya $400,000 za Marekani, zinaendeleza ujumuishaji wa kifedha, upatikanaji wa taarifa za kuaminika kwa wakulima wadogo, na haki za kisheria za umiliki wa ardhi kwa jamii zilizotengwa.


Kutana na Washindi

Kikundi cha wanawake wakiwa wameketi wakifanya mazungumzo.

ChamaChat cha Ujuzi Craft LTD | Kenya

Mfumo wa usimamizi wa Chama wenye chatboti au programu inayoiga mazungumzo na inayoshirikisha mazungumzo baina ya wanachama na kutoa majibu ya sauti kwa Kiswahili kupitia Ujumbe mfupi (SMS) na Whatsapp. Inaunganishwa na kiolesura cha programu-tumizi ya Malipo ya kikundi, yaani API ya M-Pesa. Wanachama wanaweza kushirikiana na chatboti ya msimamizi wa Chama kwenye utendaji kazi mbalimbali, ikijumuisha kuangalia salio, maombi ya mkopo na kupokea taarifa za akaunti.

Mwanamke anashikilia viazi vitamu vya rangi ya chungwa kwenye shamba

Kiazi Bora ya Sustain Earth's Environment Africa | Tanzania

Kiazi Bora, hutumia programu ya sauti inayowafahamisha wanawake wanaoishi katika mazingira magumu na wanaoishi katika maeneo ya vijijini na jamii zilizotengwa za Tanzania kuhusu thamani za lishe ya Viazi vitamu vyenye rangi ya chungwa/njano (OFSP), ujuzi wa kilimo ili kupata mazao bora, na upatikanaji wa soko wa kina wa bidhaa za chakula ghafi au zilizosindikwa za OFSP, kupitia programu ya seti ya data ya sauti.

Wezesha

Wezesha na Kabambe ya Chuo cha Westminster, U.K| Chuo cha Moi, Kenya| Chuo cha Kiufundi cha Kenya | Chuo cha Western Michigan, USA.

Ni boti ya sauti ya Kiswahili ya simu ya mkononi ambayo haitegemei muunganisho wa intaneti. Imeandaliwa kwa ushirikiano na wakulima wadogo wanawake wa vijijini nchini Kenya kama chanzo mbadala cha taarifa za kilimo. Kwa kutumia seti za data za Mozilla katika Kiswahili, boti hii ya mazungumzo ya simu ya mkononi inaweza kutumika kwenye simu za kawaida (kabambe) na simu janja na wakulima wadogo vijijini. Boti hii shirikishi ya Kiswahili inaendeshwa na hifadhidata ya maswali yanayoulizwa mara kwa mara kutoka kwa wakulima wadogo wadogo wanawake, kikundi kilichotengwa kidijitali. Imechochewa na ujuzi uliopo, kukubalika kwa teknolojia za simu katika maeneo ya mashambani nchini Kenya.

Picha ya wanaume wawili wanaomtibu ng 'ombe mgonjwa

LivHealth Kiswahili Corpus ya Badili Innovations | Kenya

LivHealth Kiswahili Corpus inalenga kuwezesha jamii kutambua kwa usahihi magonjwa ya mifugo na kupata afua kwa wakati kutoka kwa watendaji waliohitimu. Kwa kutumia Uchakataji wa Lugha Asilia (NLP), Kujifunza kwa Mashine (ML), na Akili Bandia (AI), mradi utajenga miundo ya Kiswahili ya maandishi-hadi-sauti kwa ajili ya kusambaza taarifa za magonjwa kwa jamii zilizotengwa. Wakifanya kazi kwa karibu na washirika wao, Kituo cha One Health Center in Africa(OHRECA) chenye makao yake ILRI, wataimarisha utendaji wa mfumo wa LivHealth ili kuwezesha jamii za wenyeji kupata taarifa hitajika za magonjwa kwa urahisi na kwa Kiswahili.

Picha ya wanaume wawili wakiangalia kifaa cha rununu wakati wa mazungumzo

Imarika ya Chuo cha Strathmore | Kenya

Imarika ni boti ya mazungumzo inayotoa huduma za ushauri wa hali ya hewa kidijitali katika lugha ya Kiingereza na Kiswahili ambayo itasaidia wakulima wadogo kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa. Mradi huu unalenga kukabiliana na hatari ya wakulima kukabiliwa na hali ya hewa isiyotabirika kutokana na kukosekana kwa utabiri wa hali ya hewa unaoweza kufikiwa, wa kutegemewa na wa eneo. Upatikanaji wa taarifa za hali ya hewa ni tofauti sana katika Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na kwa kawaida ni utabiri wa hali ya chini ya usahihi wa kitaifa au wa kikanda unaotangazwa kwenye redio na/au TV. Mradi hasa unatarajia kuwahudumia wakulima wadogo ambao mara nyingi wana ufikiaji mdogo wa huduma za ushauri wa hali ya hewa zilizowekwa ndani kutokana na vizuizi kama vile kupenya polepole kwa teknolojia au kutojua kusoma na kuandika kwa dijiti.

Picha ya nembo iliyo na kipaza sauti

Paza Sauti ya Tech Innovators Network Ltd | Kenya

Mradi huu unatengeneza boti ya mazungumzo na huduma ya mwingiliano ya mwitikio wa sauti ambayo itatoa huduma zinazowezeshwa kwa sauti katika kikoa cha usajili wa biashara na kuongeza ufahamu kuhusu matumizi ya dhamana (usalama) kuwezesha kupata mkopo nchini Kenya. Lengo kuu ni kuongeza ujuzi wa kifedha kuhusu mali zinazohamishika kama dhamana, hasa kwa wanawake katika biashara, na hasa kilimo, kwa madhumuni ya kupata mikopo. Ingawa kumekuwa na ongezeko la urahisi wa kupata mikopo, wananchi wengi bado hawajui uwezo wao wa kupata mikopo zaidi kutokana na kutumia mali zinazohamishika kama dhamana. Mradi huu utakuwa mwendelezo wa ushirikiano unaoendelea tayari na Business Registration Service - BRS (Shirika la serikali) nchini Kenya katika kikoa cha ujumuishaji wa kifedha, ambacho huhudumia umma wa Kenya.

Picha ya nembo ya shirika, inayoonyesha maandishi na sifa za utambuzi wa sauti

Kiswahili Text and Voice Recognition Platform (KTVRP) kwa Ushauri wa Kilimo na Huduma za Kifedha kwa Wakulima Wadogo ya Duniacom Group, LLC| Tanzania / Marekani

Wengi wa wakulima wadogo nchini Tanzania wana uwezo wa kuwasiliana kupitia lugha ya Kiswahili na lahaja zake pekee. Jukwaa la maandishi na sauti linalopatikana katika lugha ya watu wasiohudumiwa (yaani, Kiswahili) litakuwa ufunguo wa ufikiaji mpana, kupitishwa na matumizi ya ushauri wa kidijitali ya kilimo na huduma za kifedha nchini Tanzania. Lengo ni kuandaa jukwaa la utambuzi wa maandishi na sauti ambalo litawapa wakulima wadogo katika mnyororo wa Thamani wa Mahindi Tanzania na huduma za kidijitali za kifedha na zisizo za kifedha za kiotomatiki kwa kuzingatia eneo, maeneo ya ikolojia ya kilimo na mzunguko wa mazao. Kulingana na data iliyogawanywa kwa jinsia kutoka kwa awamu ya majaribio, inategemewa kuwa wengi wa washiriki watakuwa wanawake.

Picha ya nembo ya shirika

Haki des femmes by Core23Lab | Democratic Republic of Congo
Haki des femmes itatumia teknolojia ya sauti kutoa ufikiaji wa taarifa za kisheria na usaidizi kwa wanawake katika majimbo ya Katanga na Lualaba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ili kuhakikisha wana haki ya kupata, kutumia, kurithi, kudhibiti na kumiliki ardhi. Wanawake wengi nchini DRC mara nyingi hupoteza uwezo wao wa kumiliki ardhi baada ya kufiwa na wapendwa wao au waume zao kutokana na kukosa ufahamu wa haki za ardhi. Suluhu hili itasaidia wanawake kupata taarifa na usaidizi wa kisheria katika kupata haki zao za ardhi kwa lugha ya Kiswahili.

Msaada huu unatolewa na Shirika la Gates kwa ushirikiano na Ofisi ya Jumuiya ya Madola na Maendeleo ya Kigeni (FCDO) na GIZ, kama jibu la ufahamu unaozingatia jinsia na jamii katika maendeleo ya teknolojia. Hatimaye, linakuza matumizi ya data ya sauti ya chanzo huria kwa bidhaa zinazounga mkono ushirikisho wa jamii zote katika ushirikiano.