Huu ni wasifu wa Fair EVA, mshindi wa tuzo ya Mfuko wa Teknolojia wa Mozilla. Fair EVA inajumuisha washirika wa programu huria wanaotafiti upendeleo katika muundo na matumizi ya bayometriki ya sauti.



Pengine umesikia hii hapo awali, "Simu hii inaweza kufuatiliwa au kurekodiwa kwa uhakikisho wa ubora na madhumuni ya mafunzo". Pengine ulikuwa unapiga simu katika kituo cha huduma kwa wateja cha benki, kampuni ya bima, au mtoa huduma mwingine yeyote. Ingawa hii inaweza kuonekana kama utaratibu wa kawaida, jambo lisilojulikana ni kwamba sauti yako inaweza kuwa ilitumika kutambua na kuthibitisha stakabadhi zako.

Hii inajulikana kama matumizi tulivu ya bayometriki ya sauti ambapo sauti ya mpigaji hutumika kuthibitisha utambulisho wake. Makampuni na vituo vya kupiga simu vinavyotumia teknolojia hii vinahitaji sekunde 20 pekee za sauti ya mazungumzo ya kawaida ili kuthibitisha.

Hali tofauti ni matumizi hai ya bayometriki ya sauti, ambapo mtumiaji anahitajika kusema kifungu fulani ili kuwezesha huduma za jukwaa. Kwa mfano, kaulisiri “Katika Safaricom, sauti yangu ni nenosiri langu,” hutumika kama nenosiri la sauti kufikia vipengele vya pochi ya simu kwa watumiaji wa M-Pesa nchini Kenya.

Mahitaji ya huduma salama za kidijitali yanapoongezeka, wanateknolojia wanageukia bayometriki ya sauti katika uthibitishaji wa mtumiaji. Ingawa hitaji la kutambua watu limekuwepo kila wakati, teknolojia ya uthibitishaji wa mzungumzaji ya sauti inatokana na upekee wa sauti ya mwanadamu: Sauti ya kila mtu ina wasifu tofauti, inayofanya kazi kama alama ya vidole.

Kitambulisho cha Sauti hutoa ufikiaji rahisi wa mifumo ya kidijitali bila ugumu wa kukumbuka nenosiri. Pia hutoa njia mbadala ya kutumia miundo ya kuona, na inasaidia katika hali ya viwango vya chini vya kusoma na kuandika. Voiceprint kwa sasa inatumika kama kipengele cha usalama wa nyumbani, katika programu za benki, na katika kuchakata madai ya bima. Nchini Mexico, mojawapo ya taasisi kubwa zaidi za kifedha, BBVA, hutumia bayometriki za sauti kama uthibitisho wa uhai kwa wastaafu wanaopata mafao yao.

Walakini, jamii ya karibu ya Kitambulisho cha Sauti - gumzo za utambuzi wa usemi kama vile Siri, Alexa, Google Assistant - zinakabiliwa na upendeleo mkubwa wa kabila, haswa katika kugundua lafudhi na matamshi ya watu wasiozungumza Kiingereza. Je, upendeleo huu pia unaweza kupata njia yake katika huduma za kibayometriki za sauti? Wiebke Toussaint Hutiri, kiongozi wa mradi katika Fair EVA anatabiri mwelekeo wa kutia wasiwasi, ambao unaweza kuwatenga zaidi watumiaji waliotengwa katika utumiaji wa huduma zinazolindwa na bayometriki za sauti, kuongeza uwezekano wa kuingiliwa, au kuongeza udakuzi na aina nyingine ya ubaguzi.

Hutiri anaona upendeleo kama uendelezaji wa unyanyasaji usio wa haki, "...ambao husababisha utendaji tofauti wa teknolojia kwa watumiaji tofauti. Aina hii ya upendeleo inaweza kuwa na sababu tofauti za kutokea, lakini sababu fulani ya ukaidi ni wakati wa ukuzaji wa kujifunza kwa mashine. Ingawa madhara haya kwa kiasi kikubwa hayakutarajiwa, bado yanaweza kusababisha baadhi ya makundi ya watu kukumbwa na madhara yasiyolingana.”

Anaongeza, "Kinachovutia katika fani hii ya teknolojia ni kwamba sauti inakuwa sehemu ya kwanza ya ufikiaji, [na kwayo] upanga wenye ncha mbili. Kwa upande mmoja, tunaweza kuuona kama kipengele cha usalama ambacho hutoa ugunduzi wa uvamizi - kulinda watu wasioidhinishwa katika ufikiaji, lakini pia unaweza kuwanyima kuingia kwa watu wanaopaswa lakini hawatambuliki kwa usahihi. Upendeleo angalau unaweza kuzuilika, ndiyo maana tunatafuta njia za kuutambua na kuushughulikia kwa kutumia bayometriki za sauti."

Zaidi ya hayo, ana nia ya kutofautisha kati ya upendeleo na ubaguzi. Anafafanua ubaguzi kama kitendo cha kimakusudi cha kuonyesha chuki, "[...] mawazo potofu kulingana na sifa nyeti au zinazolindwa za watu binafsi." La kutisha zaidi ni kwamba bayometriki za sauti pia zinatumiwa kwa njia isiyo na uadilifu ili kuongeza udakuzi katika baadhi ya magereza nchini Marekani, ambapo data ya simu kati ya wafungwa na wapendwa wao inarekodiwa, kuhifadhiwa na kuchambuliwa, kwa kisingizio cha utoaji vipengele vya ziada vya usalama. Data hii inaweza kutumika kutambua watoto, familia, marafiki, au mitandao mingine ya nje ya wafungwa.

Kufuatilia Upendeleo

Je, bayometriki za sauti ni sahihi kwa kiasi gani katika kumtambua mtumiaji, na je, kuna dosari katika ishara zinazofaa za utambuzi wa mtumiaji za upendeleo? Hutiri anasema ishara zinazojulikana hujitokeza wakati wa kujibu maswali haya: "Teknolojia hizi zimeundwa kwa ajili ya akina nani, na ni dhana zipi zimeafikiwa katika mchakato wa kubuni?"

Kwa akina nani: Hatua hii muhimu ya mlinganyo inahitaji ukaguzi wa kidemografia wa mahali ambapo bidhaa hizi zinatengenezwa kwa sasa na wapi programu zinatumwa. Timu ya Fair EVA kwa sasa inaunda hifadhidata ya wachuuzi na watoa huduma wanaotumia teknolojia hizi kuunda programu za kitambulisho cha sauti. "...Kujaribu tu kufanya ufuatiliaji tayari kuna changamoto," Hutiri anaelezea. "Kikwazo kingine ni kwamba teknolojia ya sauti yenyewe ni yenye matumizi mahsusi sana. Je, ni dhana au vipengele gani ambavyo wabunifu wa teknolojia wamejumuisha katika programu ili kushughulikia mabadiliko ya sauti? Kwa mfano; rangi, jinsia, rika, ugonjwa, au hata hisia?"

“Upendeleo wa bayometriki ya sauti ni wenye muktadha asili na matumizi mahsusi. Iwapo tutaifanyia majaribio teknolojia bila kujua ni hali zipi zimezingatiwa na wasanidi programu, basi tutaanguka katika mtego wa kukisia. Badala yake, anapendekeza "... uwazi wa muundo wa bidhaa na ufikiaji wa tathmini za majaribio."

Wiebke Toussaint Hutiri - Fair EVA

Kwa sababu programu tofauti husheheni miundo tofauti, timu ya Hutiri inasuta muundo wa kimo-kimoja-husitiri kila kitu katika kutafiti upendeleo. “Upendeleo wa bayometriki ya sauti ni wenye muktadha asili na matumizi mahsusi. Iwapo tutaifanyia majaribio teknolojia bila kujua ni hali zipi zimezingatiwa na wasanidi programu, basi tutaanguka katika mtego wa kukisia. Badala yake, anapendekeza "... uwazi wa muundo wa bidhaa na ufikiaji wa tathmini ya majaribio."

Kwa mfano, "Katika hali ambayo hatujui jinsi teknolojia ilivyojaribiwa - lakini bidhaa inarekodi usahihi wa 98%, haijulikani iwapo usahihi ni kuwaweka wavamizi nje ya jukwaa au usahihi upo kwenye utambulisho sahihi wa watumiaji. Kuna maelewano kati ya haya mawili, na makosa katika matukio yote mawili huleta athari, na uwezekano wa kujitokeza kwa upendeleo.

Kutathmini Upendeleo

Ili kutathmini upendeleo, timu ya Hutiri inaunda zana yenye miongozo ya kufanya utathmini wenye muktadha mahsusi wa seti za data, na kuunda maktaba ya Python ili kukagua upendeleo wakati wa uundaji wa bayometriki ya sauti. "Tuligundua kuwa hatuwezi kuunda seti ya data ambayo itashughulikia kila hali inayowezekana, lakini badala yake, tuelekeze jinsi tathmini inapaswa kufanywa. Kisha tunaweza kutumia maarifa kutoka kwa utengenezaji wa mwongozo wa tathmini ili kupendekeza viwango vya kuripoti jinsi utendaji wa teknolojia unapaswa kuwasilishwa kwa watumiaji," Hutiri anafafanua.

Timu yao kwa sasa inaandaa wito wa mchango wa sauti wa umma kwa data iliyokusanywa na Google Assistant na kutumia data hiyo kuunda seti ya data ya tathmini.