Picha ya tukio la MozFest House: mjini Amsterdam, mapema mwaka huu
Picha ya tukio la MozFest House: mjini Amsterdam, mapema mwaka huu

____

Tukio lifwatalo la MozFest litatumia vizuri nafasi ya kuleta pamoja wanateknolojia maarufu wa Afrika; tukio hili limepangwa mnamo tarehe 21 na 22 Septemba, 2023 katika Mkahawa almaarufu kwa jina la Nairobi Shamba House Cafe

(NAIROBI, KENYA | JULAI 27, 2023) – Mwezi wa Septemba mwaka huu, Tamasha ya Mozilla Festival House nchini Kenya itakabiliana na masuala makuu kupitia majadiliano kuhusu teknolojia zinazoibuka barani Afrika, kama vile ukusanyaji na utumizi wa data na udhibiti wa AI (akili bandia).

Nyumba ya MozFest: Kenya itajumuisha kazi ya Africa Innovation Mradi, kuwezesha nafasi kwa jamii mbalimbali kukusanyika na kupeana ujuzi, kujadiliana, na kuunda ushirikiano unaozingatia maendeleo na usimamizi wa kiteknolojia katika kanda ya Afrika ya Mashariki na Kusini. Tukio hilo litafanyika Septemba tarehe 21 na 22 mwaka wa 2023 katika mkahawa wa Shamba House jijini Nairobi.

MozFest House: Kenya ni mwakilisho wa tamasha ya kikanda ya Mozilla, mkusanyiko wa kila mwaka wa wanateknolojia, watafiti, watunga sera, wanaharakati, na wengine ili kuchunguza masuala yanayohusiana na mtandao unaozingatia haki za binadamu na AI inayoaminika.

Tukio hilo linakuja wakati ambapo kuna mvutano kati ya uwezo mkubwa wa kiteknolojia ambao haujadhibitiwa, na jitihada za kuweka teknolojia zinazoambatana na sheria katika bara zima. Hivi sasa, wanateknolojia nchini Kenya wanapigania hali bora ya kazi na malipo bora. Kwa sasa, masuala tatanishi katika ukusanyaji na matumizi ya data za kidijitali, yanazungumziwa na umma, yakionyesha uhusiano kati ya jukumu la kampuni maarufu za kiteknolojia barani Afrika na historia ya kikoloni.

"MozFest House Kenya ni mkutano wa kikanda wa kujadili umuhimu wa maadili ili kutetea kile kilicho haki, kuhusiana na usalama wa kidijitali, haki zinazohusiana na matumizi ya kidijitali, uwajibikaji katika mambo ya teknolojia, na AI ya kuaminika barani Afrika."

Chenai Chair, Afisa Mwandamizi wa Programu, Afrika Mradi

Ili kukata mizizi ya mazoea yasiozingatia ubinadamu, MozFest House: Kenya itashirikisha mazungumzo ya ujasiri na hatua thabiti za kujenga teknolojia zinazofuata maadili bora, usawa, na ubinadamu. Kwa kweli, MozFest House Amsterdam mapema mwaka huu ilifungua njia kama mahali pa kuzindua agano la kwanza la Amsterdam la kulinda vijana mtandaoni.

MozFest House Kenya itakuwa na:

  • Zaidi ya vikao 20 vitakavyokuwa na mada hii, “Mobilizing African Communities for Trustworthy AI.” Vipindi hivi vya maingiliano vitazingatia masuala muhimu katika Afrika ya Mashariki na Kusini, kama vile usalama wa kidigitali, haki zinazohusiana na matumizi ya kidigitali, uwajibikaji katika majukwaa, na haja ya udhibiti wa mtandao. Vikao vitatangazwa mwezi Agosti.
  • Hotuba muhimu na washiriki kutoka kwa harakati maarufu kote Mashariki na Kusini mwa Afrika — wakiwemo wataalam wa sera za kiteknolojia, wasanii na wanaharakati wa masuala ya kiteknolojia. Matukio ya zamani ya MozFest yamejumuisha wasemaji kama Frances Haugen, Bitange Ndemo, na Tim Berners-Lee. Wazungumzaji watatangazwa mwezi Agosti
  • Maonyesho, mafunzo, hakathoni (maonyesho ya usanidi programu), na programu nyinginezo ambazo hasababisha kuwepo kwa AI barani Afrika

Tiketi ni bure, lakini unahitajika kujisajili

Anavyosema Chenai Chair, Afisa Mwandamizi wa Programu, Afrika Mradi

"MozFest House Kenya ni mkutano wa kikanda wa kujadili umuhimu wa maadili ili kutetea kile kilicho haki kuhusiana na usalama wa kidijitali, haki zinazohusiana na matumizi ya kidijitali, uwajibikaji katika teknolojia, na AI ya kuaminika barani Afrika. Tamasha hii ni mkusanyiko wa kwanza wa wanaharakati, wasanii, wanateknolojia, na waelimishaji katika harakati mbalimbali za kimataifa zinazopigania ulimwengu na mtandao unaozingatia ubinadamu."

Anasema Sarah Allen, Mkurugenzi Mwandamizi wa MozFest:

"MozFest Kenya ni sherehe ya kazi ambayo inafanyika ndani ya nchi kutetea na kujenga teknolojia za umoja na zinazofuata maadili mema. Kenya inaongoza kwa uvumbuzi wa ndani na udhibiti wa mtandao — na tunataka kuchangia katika kasi hiyo."


Maudhui yanayohusiana