Sisi ni nani

Shirika la Mozilla linafanya kazi ili kuhakikisha kuwa mtandao unabaki kuwa rasilimali ya umma iliyo wazi na ambayo sisi sote tunaweza kuifikia.

Hali bora ya mtandao

Mtandao wenye hali bora ni ule ambao unzingatia ufaragha, uwazi na ujumuishaji wa makundi yote. Haya ni maadili ambayo Mozilla imethamini kutoka kuanzilishwa kama ilivyo kwenyeManifesto ya Mozilla.

Mozilla inaamini kwamba sisi sote tuna jukumu la kuelewa na kulinda hali bora ya mtandao. Kwa sababu hii, Mozilla Foundation inalenga hasa kuchochea uanaharakati unaoibuka wa watumizi wa intaneti, wanateknolojia, watafiti na wanaharakati ambao wamesimama na kupigania mtandao wenye hali bora kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Ikoni yenye mishale 4 inayoenda pande tofauti

Soma zaidi kuhusu sera yetu ya faragha hapa.

Picha yenye mandharinyuma ya zambarau, diski 2 na maneno "Akili Bandia"

Mifumo ya AI inayoaminika

Kazi kubwa ya za ujenzi wa harakati za Mozilla zinalenga kukuza AI inayoaminika.

Mozilla ina mradi wa jinsi ya kufanya kazi kuelekea AI ambayo inaboresha maisha ya wanadamu, badala ya kuwadhuru. Tunaiita ‘AI ya kuaminika’ na hii inaongoza sehemu kubwa ya kazi yetu.

Tangu 2019, wengi wetu katika Mozilla — pamoja na mamia ya washirika na washiriki — tumekuwa tukichunguza maswali: Tunamaanisha nini kwa ‘AI inayoaminika’? Na, tunataka kufanya nini kulihusu?

Ikiwa tunataka intaneti yenye afya na jamii ya kidijitali yenye afya, tunahitaji kuhakikisha kuwa mfumo wa AI unaaminika. AI, na idadi kubwa ya data inayoichochea, ni msingi wa jinsi kompyuta inavyofanya kazi leo. Iwapo tunataka programu, mitandao ya kijamii, vifaa vyetu na serikali itutumikie kama watu—na kama raia—tunahitaji kuhakikisha jinsi tunavyounda na AI ina mambo kama vile faragha na usawa ndani yake. kutoka mwanzoni.

Ikoni yenye mishale 4 inayoenda pande tofauti

Soma zaidi kuhusu nadharia yetu ya mabadiliko ya AIhapa.