Je, Ushirika wa Mozilla ni nini?

Siku hizi mtandao wa intaneti umeenea kote: Unaunda uchumi, unashawishi serikali, na mabilioni ya watu wanautegemea.

Intaneti iliyoenea ina uwezo wa kuinua jamii — inaweza kukuza demokrasia, masoko huria, na uhuru wa kujieleza. Lakini pia inaweza kukuza ubaguzi, ufuatiliaji wa watu wengi, na habari potofu.

Zaidi kuliko hapo awali, tunahitaji harakati za kuhakikisha kuwa mtandao unaendelea kutumiwa kwa kusudi nzuri. Washirika wa Mozilla ni wanaharakati, watafiti huria, wahandisi, na wataalamu wa sera za teknolojia ambao wanafanya kazi kwenye mstari wa mbele wa harakati hiyo. Washirika hubuni mawazo mapya kuhusu jinsi ya kukabiliana na vitisho vinavyojitokeza na changamoto zinazokabili mtandao wenye maadili mema.

Washirika wa Mozilla wanajitahidi kuunda modeli mpya za utawala wa data, kuhakikisha kuwa akili ya bandia inawajibika, kukomesha kuenea kwa habari potofu na kuendeleza utambuzi wa sauti wa lugha za jamii zilizotengwa. Kama sehemu ya jumuiya mbalimbali na ya kimataifa, Washirika wa Mozilla wana fursa ya kujifunza na kuchangia katika njia mbalimbali za kukabiliana na vitisho vinavyojitokeza na changamoto zinazokabili mtandao wenye maadili mema.

Washiriki waliokaribishwa na mashirika ya kiraia

Amelia

Mtandao huru

Washirika hufanya kazi katika uwanja wa teknolojia inayozingatia maslahi ya umma, huku wakishughulikia masuala kama vile faragha, usalama, na ujumuishaji mtandaoni. Wanaharakati hawa wa mtandao huria wamekita mizizi katika haki za binadamu na mashirika yanayoongoza ya kiraia duniani kote, wakishiriki uzoefu wao wa utaalamu wa kiufundi.

Brian Obilo

Teknolojia + Jamii

Washirika hawa wanajenga uwezo katika makutano ya teknolojia na jamii. Wanashirikiana na mashirika ya ndani ya kujenga ‘nafasi ya tatu’ ambapo mashirika muhimu ya kiraia na watu binafsi wanaopendezwa na teknolojia kushughulikia masuala katika makutano ya teknolojia na jamii.

Kukutana na Washirika

Washirika wanaoshirikiana na Mozilla

Britone

Common Voice

Wataalamu hawa wa teknolojia za sauti za kujifunza wanakuza juhudi za ukusanyaji wa data huria na kutoa ushauri wa kiufundi ili wasaidie utambuzi wa usemi na uigaji wa usemi wa lugha za eneo la Afrika Mashariki. Washirika hawa ni sehemu ya mradi wa Mozilla unaoitwa Common Voice.

Kukutana na Washirika

Kathy Pham

Kutengeneza Teknolojia Inayozingatia Maadili

Kama sehemu ya Mashindano ya Mozilla ya Kutengeneza Teknolojia Inayozingatia Maadili, washirika hawa wanasaidia mbinu zinazoelekea kufanikiwa za kuunganisha maadili katika elimu ya sayansi ya kompyuta na kuwawezesha kikundi kipya cha wataalamu wa teknolojia wanaohitimu kuleta mawazo kamili ya kubuni bidhaa za teknolojia na kusababisha mabadiliko ya utamaduni katika sekta ya teknolojia.

washirika wa sera za teknolojia

Washirika Wakuu: Sera ya teknolojia

Washirika hawa Wakuu ni wataalam wa sera wanaofikiria kwa kina kuhusu masuluhisho ya ubunifu lakini mahususi ya sera zinazohitajika ili mfumo ikolojia wa AI (mifumo ya akili bandia) uaminike zaidi na wanaoangalia masuala haya ya sera kutoka kwa mtazamo wa kushirikiana na nyanja zingine za uanaharakati.

Kukutana na Washirika

Deborah Raji

Washirika Wakuu: AI Inayoaminika

Washirika hawa ni wataalamu wa eneo wanaoshirikiana na Mozilla kufikia lengo la ulimwengu ambamo AI inayoaminika inaboresha maisha ya wanadamu. Kazi yaoinazingatia kukabiliana na masuala ya upendeleo, uwazi duni, na usimamizi wa data ambao kwa sasa huzuia uhalisia huo.

Kukutana na Washirika

Tukio la Ushirika

Tangu mwaka wa 2011, shirika la Mozilla Foundation limeunda na kuendesha shughuli za mipango ya Ushirika na Tuzo wakishirikiana na wafadhili mbalimbali ili kukuza teknolojia mbalimbali za ubunifu, na vipaji katika ushirikiano baina ya teknolojia na mashirikia ya kijamii.

Ushirika wa Mozilla hutoa muda, rasilimali, zana, jamii, na kusaidia sana watu wanaojenga ulimwengu wa kidijitali unaozingatia maslahi ya wanadamu zaidi. Wakati wa muda wao wa kushika cheo, Washirika hutumia ujuzi wao — katika teknolojia, katika sera, katika utafiti, katika harakati — kufanya utafiti wa uchunguzi, kuendeleza mifumo ya sera, kujenga jumuiya, na hatimaye kuweka msingi wa mtandao huria na unaojumuisha wote.

Kando na msaada wa malipo na misaada ya kila mwezi, washirika huwa sehemu ya jamii ya Mozilla na kupata rasilimali zetu na kuweza kutumia mitandao mbalimbali. Misaada inajumuisha:

  • Ubunifu wa Athari: Kwa kushirikiana na Mozilla, kila Mshirika anaunda mpango wa mradi — akielezea nadharia ya mabadiliko pamoja na vipimo vya athari.
  • Msaada wa mtu binafsi na marika: Washirika wote wana fursa ya kupokea ushauri na mwongozo kutoka kwa wafanyakazi na washirika walio katika shirika la Mozilla. Wanapata ujuzi kama vile AI na usimamizi wa jamii na usimamizi wa mradi. Washirika pia wanaripoti kwa afisa wa mpango na watakuwa na mikutano ya ana kwa ana inayopangwa mara kwa mara.
  • Jumuiya: Uhusiano na viongozi wenye nia kama hiyo, fursa za kushirikiana na mashirika ya washirika, wanachama wa zamani, na wafanyakazi wa Mozilla, na ushirikiano wa wahusika kutoka nyanja mbalimbali ili kusaidia mradi wao.
  • Mtandao na Rasilimali- Kuanzia miradi kama vile Common Voice hadi utaalamu — na uwezo wa — Maono ya Mozilla na timu za utetezi , Mozilla ina mipango mbalimbali na zana ambazo washirika wanaweza kutumia ili kuendeleza kazi zao.
  • Ukuzaji wa Mradi: Timu ya Mawasiliano na mahusiano ya umma ya Mozilla hutoa msaada mbalimbali kwa washirika ili waeleze kazi zao kwa watazamaji wengi, kukiwemo na kuandika, kuhariri, kutunga maudhui, kuelezea vyombo vya habari dhamira yao, kuwezesha matukio ya kuzungumza, na kushiriki na watazamaji wa tovuti ya Mozilla na orodha ya wanaotumiwa barua pepe.
  • Kuonyesha Kazi: Mozilla ina tamasha ya kila mwaka inayoitwa MozFest ambayo huleta pamoja wasanii, wanaharakati, wachunguzi, na wajenzi wanaofanya kazi kutoka duniani kote wanaojitahidi kuhakikisha kuwa tuna mtandao wa intaneti unaozingatia maadili mema. Tukio hili linatoa nafasi na fursa ya kukutana, kuwezesha au kuchagua kwa njia inayosaidia washirika kuwasilisha masuala muhimu sana kwao na jamii zao.

Je, mbona uwe Mshirika?

Washirika wa Mozilla wanaalikwa watumie ushirika kama jukwaa la kufanya kazi muhimu kwao na ya mtandao wenye maadili mema. Washirika wa Mozilla wana fursa ya kujifunza na kuchangia katika masuala mbalimbali na mbinu za kuhakikisha kuwa mtandao unaendelea kutumiwa kwa kusudi nzuri. Kama Mshirika:

Nilikuwa nikifanya kazi katika New York Times kama mwandishi wa habari wa data na nilikuwa nafanya kazi usiku na wikendi, huku pia nilisaidia vikundi kufikiria juu ya ufuatiliaji na usalama wa kidijitali na usafi na usalama. Nilizungumza na watu wachache na wakasema, kuna ushirika fulani wa Mozilla unaopaswa kuangalia. Kwa hiyo nilijiambia, nitatuma ombi na ombi langu likikubaliwa, nitajitolea sana katika kazi hiyo, labda nitaridhika zaidi kufanya mema na kutumikia jamii kwa njia hiyo.... Siongezi chumvi ninaposema limebadilisha maisha yangu."

Matt Mitchell, Mshirika wa Mozilla wa 2017-2018

ikoni ya moyo

Je, unataka kuunga mkono kazi ya ajabu ambayo Washirika wanafanya? Kama shirika la linalokaribisha au mfadhili, unaweza kujiunga nasi katika kuhakikisha kuwa mtandao unaozingatia maadili mema. Jua jinsi ya kushirikiana nasi.