Picha iliyo na taarifa kuhusu Tamasha la Sauti ya Kawaida DRC. Tamasha litakalofanyika Lubumbashi tarehe 24 hadi 25 Mei na zawadi zenye thamani ya $300 USD au 693,000 CDF zitashinda.

Watakaohudhuria watajifunza jinsi ya kuchangia kwenye Common Voice na kushindana katika uandishi unaojumuisha jinsia.

(LUBUMBASHI, DRC | JUMATATU, MEI 22)Washiriki wa Mozilla Common Voice, kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Nouveaux Horizons na Deep Learning Indaba – tawi la DRC, wanaalika wanafunzi na wasomi kwenye Tamasha ya Common Voice jijini Lubumbashi mnamo tarehe 24 - 25 Mei.

Tukio hili, linalolenga kukuza jumuiya ya Common Voice na seti ya data, ni tamasha la pili la Kiswahili mwaka huu. La kwanza lilifanyika Mombasa, Kenya. Tamasha hili litaimarisha jumuiya ya lugha ya Kiswahili na teknolojia inayojumuisha jinsia ambayo inaleta lugha ya Kiswahili mtandaoni kwa njia ya usawa.

Anasema Rebecca Ryakitimbo Mwimbi, mwenyeji wa tamasha ya Mozilla Common Voice: “Wanawake ni sehemu muhimu ya jumuiya ya kiteknolojia na lugha ambayo mradi wa Common Voice wa Kiswahili unanuia kushirikisha na kuwezesha. Kuna mengi ya kuhitajika katika teknolojia ya sauti linapokuja suala la ushirikishwaji wa kijinsia kwa ushiriki halisi na ushirikishwaji wa maana wa wanawake. Tunalenga kuchangia mabadiliko kwa kuandaa tamasha hili.”

Common Voice ndiyo mkusanyiko wa data ulio na wingi wa lugha mbalimbali uliopo, unaoendeshwa na sauti za wachangiaji wa kujitolea duniani kote.

Washiriki katika tamasha wanaweza kuwa:

  • Wachangiaji wa sauti - watu binafsi wanaochangia sauti zao kwenye jukwaa
  • Waundaji sentensi - watu ambao hutunga sentensi ambazo hutumika kwenye mfumo wa Sauti ya Kawaida
  • Wathibitishaji wa sauti - watu binafsi wanaosikiliza sauti zinazotolewa na kuthibitisha data
  • Mtumiaji wa seti ya data ya sauti (msanidi wa programu) - watu binafsi wanaotumia data kutengeneza programu

Tukio hili la siku mbili litajumuisha utangulizi wa jukwaa la Common Voice kwa wanaoweza kuwa wathibitishaji wa sauti au wachangiaji wa sauti. Siku ya pili itaangazia shindano la uandishi la ufeministi ili kuratibu maudhui ya ufeministi kwa jukwaa, kwa kuzingatia Mpango wa Utekelezaji wa Jinsia wa Common Voice.

Tuzo za hadi 693,000 CDF ($300 USD) zitatangazwa mwishoni mwa siku ya pili kwa washindi wa shindano la uandishi na shindano la mfano.

Wasiliana na waandishi wa habari: Shandukani O. Mulaudzi, [email protected]


Maudhui yanayohusiana