Seti za data za Common Voice hukusanywa na kusambazwa ili kusaidia kuhakikisha kwamba teknolojia za sauti zinaweza kutumika kwa anuwai ya wazungumzaji wa kimataifa iwezekanavyo. Ingawa timu yetu ndogo inazungumza lugha kadhaa, hatuna utaalamu wa kufanya maamuzi sahihi ya lugha kuhusu lugha zaidi ya 120 kwenye mfumo wetu. Common Voice daima imekuwa juhudi ya jumuia na tunataka kufanya kazi kwa karibu zaidi na jumuia za lugha zetu tunapoendelea kukua ili kukuhudumia.
Tunazindua Mradi wa Mabingwa wa Lugha, uliochochewa na mipango ya awali kama vile mradi wa Mabingwa wa Kiswahili na Baraza la Wawakilishi wa Lugha. Mpango huu utahakikisha kwamba wazungumzaji wa lugha hiyo wanaendesha maamuzi ya lugha mahususi kwenye Common Voice. Kikundi hiki kitajumuisha watu wa kujitolea ambao wanaweza kutumika kama marejeleo ya msingi na mahali pa kuwasiliana kwa maswali yoyote mahususi ya lugha, maamuzi na kutusaidia kuondoa mahangaiko yoyote.
Kwa vile hili ni jukumu la kujitolea tunataka kupunguza uzito wa kazi hii ya ushauri kuwa nyepesi kwa wafanyakazi wetu wa kujitolea. Kwa sasa, tunatafuta tu watu wanaotaka kuwa sehemu ya jumuia hii na kutoa utaalamu wao inapowezekana. Kwa mfano, tunaweza kuwasiliana nawe ili tupate ushauri wako kunapokuwa na swali kuhusu tahajia ya kutumia kwa lugha mpya, ili kutusaidia kufanya maamuzi kuhusu ombi kubwa la sentensi katika lugha yako au kupata tu mawazo yako kuhusu masuala ya ubora wa mkusanyiko wa data katika lugha mahususi.
Iwapo ungependa kujiunga na juhudi hii na kuwakilisha lugha yako, tafadhali jisajili kupitia fomu hii ya mabingwa wa jumuiya ya kujieleza.
Kwa watumizi ambao hawawezi kufikia fomu hii, unaweza kututumia barua pepe kwa anwani ifuatayo: commonvoice(at)mozilla.com yenye mada "Mabingwa wa Jumuiya" na maelezo yafuatayo:
- Barua pepe: ...
- Majina na Jina la familia: ...
- Jina ya Lugha yako: ...
- Msimbo wa Lugha:
- Kanda ya wakati: ...
- Je, ungependa kuhudhuria mikutano ya jumuia ya kila mwezi/mara mbili kwa mwezi?: (Ndio / Hapana / Labda)
- Uzoefu au usuli katika lugha hii: ...
- Taarifa yoyote ya ziada au maelezo: ...
Tunataka kufanya haraka ili tuweze kujumuisha ujuzi wako wa lugha kuelekea mradi wa Common Voice, kwa hivyo tunapanga mkutano wa kuanza mwishoni mwa Septemba ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na jumuia za lugha, ubora wa data na jinsi tunavyoweza kuboresha ushirikiano ili kusonga mbele.
Iwapo unamfahamu mtaalamu wa lugha, mhandisi wa ASR (utambuzi otomatiki wa usemi), mwanaharakati wa lugha au mpenda teknolojia ya usemi ambaye unadhani angevutiwa, tafadhali mtie moyo ajisajili pia ili apate kushiriki.
Tunatarajia kufanya kazi pamoja ili kuboresha uzoefu wa jumuia zote za lugha zinazoshiriki katika mradi wa Common Voice!
Asante kwa usaidizi wako unaoendelea!