Picha ya mfano ya chatbot inayotambua sauti inayowasiliana na watu


Boti ya gumzo ya Telegram inayowezesha michango ya sauti na programu ya Android inayoweza kutumika nje ya mtandao — Miradi miwili iliyotengenezwa na wanateknolojia wa sauti kutoka Ethiopia na Italia inafanya mfumo wa Common Voice wa Mozilla kufikiwa zaidi kwa wale walio katika mazingira hafifu ya mtandao au yasiyo na mtandao.


Utendaji uliowezeshwa na sauti unazidi kuwa maarufu, lakini watu wengi hawawezi kufikia au kutumia kipengele hiki kikamilifu. Vizuizi vya lugha na ufikiaji mdogo wa mtandao wa bei nafuu unaendelea kufungia jamii zilizotengwa kutumia teknolojia kama hizo.

Seti ya data ya sauti ya chanzo huria ya Mozilla, Common Voice, inabadilisha matumizi ya lugha katika teknolojia kwa kuzipa kipaumbele lugha asili na zisizo na nyenzo. Kwa kuwaalika watu binafsi kuchangia sauti zao, jumuiya zina mchango katika kufanya programu zinazotumia sauti zijumuishwe zaidi na zipatikane katika lugha asili na lahaja. Lakini ili kushiriki kwa sasa, Common Voice inahitaji muunganisho thabiti wa intaneti, jambo ambalo ni kikwazo. Vipengele vikuu vya mchango wa jukwaa ni vikusanya sentensi na violesura vya kutamka na kusikiliza - ambavyo huruhusu watumiaji kutoa sauti zao na klipu zao kuthibitishwa.

Ili kuhakikisha kuwa kila mtu anaweza kushiriki kwa urahisi katika mpango huu, Common Voice ilialika wapenda teknolojia ya sauti Oktoba iliyopita kutoa masuluhisho yatakayowawezesha watumiaji kuchangia sauti zao katika mazingira duni yasiyo na muunganisho wa intaneti. Mpango huu uliwezekana kwa ushirikiano wetu na NVIDIA.

Anasema EM Lewis-Jong, Mkuu wa Common Voice, "Kwa kuwa na shirika kama NVIDIA - ambalo hutumia Common Voice kuunda bidhaa za kupendeza - kuwekeza tena kwenye mradi, tumeweza kuendeleza jukwaa, kushughulikia maswala halisi ya ujumuishaji na kuhakikisha kuwa faida inarudi kwa jumuiya ya chanzo huria. Miradi hii miwili iliyoshinda ni mwanzo tu.”

"Sauti inayotamkwa ni msingi wa mawasiliano na kujenga violesura vinavyotegemea sauti ni mojawapo ya changamoto ngumu zaidi za kujifunza kwa mashine. Katika NVIDIA, tunatengeneza utafiti na bidhaa muhimu katika kikoa cha sauti cha AI, na tunaunga mkono Mozilla kama sehemu ya juhudi za jumuiya ya kimataifa kupanua AI ya sauti zaidi ya lugha chache zinazowakilishwa kwa sasa."

Kari Briski, Makamu wa Rais Speech AI, NVIDIA

Timu mbili, moja nchini Ethiopia na nyingine nchini Italia, kila moja imetunukiwa USD $5000, ili kutekeleza au kuendeleza mawazo yao.

EM anaendelea, “Common Voice ni jukwaa linaloendeshwa na watu na kwa ajili ya watu. Wito huu wa wazi ulikuwa wa kuruhusu jumuiya kubuni kwa ubunifu masuluhisho ambayo yataendeleza ufikivu wa teknolojia ya sauti. Miradi miwili iliyoshinda ilikidhi vigezo vyetu vyote, kutoka kwa ufikiaji hadi muundo wa chanzo-wazi, hadi faragha, na kwingineko."

Hapo chini, kwa maneno yao wenyewe, timu hizo mbili zinazungumza kuhusu miradi yao, motisha ya kushiriki, na athari wanazokusudia kufanya.

Limon Data and Analytics | Ethiopia

Wazo letu lilichochewa na mradi wa awali ambao ulitumia boti ya Telegram kuingiliana na watumiaji na kutoa huduma za kimsingi katika hali duni ya muunganisho wa intaneti. Telegram inatumika sana nchini Ethiopia kwa hivyo tulitaka kugusa msingi wa watumiaji uliopo. Tunatumai kuwa mradi huu utahamasisha na kuwawezesha Waethiopia kuchangia sauti zao katika lugha mbalimbali zinazozungumzwa. Pia tunatumai kuwa mradi utawahimiza wasanidi programu wengine na wapenda teknolojia kuchangia na kutumia seti ya data ya Common Voice ili kubuni miundo ya mwingiliano wa sauti kwa lugha za Kiafrika. Tunaamini kuwa hii itafanya teknolojia kufikiwa zaidi, kuchangia kuondoa upendeleo wa AI, na kwa ujumla kupunguza pengo la teknolojia.

Timu yetu inajumuisha:

Amanuel Samuel Getahun: Mchambuzi wa data aliyejifundisha mwenyewe na mhandisi wa programu, anayehusika katika miradi inayotoa changamoto kwa huduma zilizopo zinazohusiana na data nchini Ethiopia. Katika Limon Data and Analytics, Amanuel hushirikiana na mashirika ya kiserikali na ya kifedha kutambulisha na kujenga upya miundo ya usimamizi na uchanganuzi wa data. Pia ni mbunifu aliyefunzwa kutoka Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Addis Ababa na mwandishi wa habari ambaye amefanya kazi katika nyanja za taaluma mbalimbali .

Mohammed Abdulkadir Mohammed: Mhandisi wa data na msanidi programu ambaye amehusika katika Limon Data and Analytics tangu kuanzishwa kwake. Mohammed alihitimu kama mhandisi wa umeme katika udhibiti wa viwanda kutoka Chuo Kikuu cha Addis Ababa na ujuzi wake unahusu utaalam wa umeme hadi kutengeneza programu na kujifunza mashine. Anaongoza shughuli na kazi ya maendeleo katika Limon ambapo anazingatia kukabiliana na ukosefu wa miundombinu ya data nchini Ethiopia.

Ruth Ghidey Gebremedhin: Mwanafunzi wa Ph.D ya Uhandisi wa Umeme katika Chuo Kikuu cha New York ambako anasomea mawasiliano yasiyotumia waya. Ana maslahi katika nadharia ya habari, mawasiliano ya kidijitali, kujifunza kwa mashine, haki ya data, na haptics - matumizi ya teknolojia inayochangamsha hisia za kugusa na kusogea. Katika Limon Data and Analytics, ameunda mikakati tofauti katika viwango kadhaa na kufanya kazi katika kubuni na kuwezesha utendaji tofauti wa algoriti.

Saverio Morelli | Italia

Mimi ni Saverio, almaarufu Sav au Sav22999 kwenye mtandao. Nina umri wa miaka 23 na ni mwanafunzi wa Sayansi ya Kompyuta katika Chuo Kikuu cha Trento nchini Italia. Nimekuwa nikipenda teknolojia kila wakati na Mozilla imerahisisha kutengeneza bidhaa zilizoleta matokeo. Kwa hivyo nilileta shauku hii nyumbani na kuwa mjenzi wa jumuiya ya Common Voice nchini Italia.

Mradi huu mahususi ulikuwa nafasi ya kupanua ubunifu wangu na kuchangia ipasavyo katika kukuza mkusanyiko wa data huria wa Common Voice. Nilianza kutengeneza programu huria ya Android "Mradi wa CV" hapo awali, na sasa nina hamu ya kutumia tuzo hii ya pesa kuboresha vipengele vya programu ya nje ya mtandao, na upatikanaji wake - na kuhimiza wasanidi programu wengine kuunda bidhaa sawia ambazo ni huria.


Maudhui yanayohusiana